Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutunza mazingira kuepuka magonjwa ya mlipuko

23 June 2026, 16:33

Mtu hawezi kuwa salama katika mazingira yasiyo safi na salama.Picha na mtandao.

Iwapo hatua za usafi wa mazingira hazitachukuliwa kwa wakati, magonjwa hayo yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii, ikiwemo kulazwa hospitalini na hata kupoteza maisha, hivyo akasisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki katika kutunza usafi wa mazingira yanayomzunguka.

Na Daniel Njau.

Wananchi wametahadharishwa kuhusu kuongezeka kwa hatari ya magonjwa ya mlipuko katika maeneo yenye mazingira machafu, wakieleza kuwa uchafu unaokusanyika kwenye makazi na maeneo ya umma unahatarisha afya za wakazi na kuchangia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko.

Wananchi hao wamesema kuwa mtu hawezi kuwa salama katika mazingira yasiyo safi na salama, kwani taka zinazotupwa ovyo na mifereji iliyoziba huongeza uwezekano wa kuzaliana kwa wadudu na vijidudu vinavyosababisha maradhi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wameeleza kuwa baadhi ya mitaa imekuwa ikikumbwa na changamoto ya usafi kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa taka, hali inayowaweka wakazi katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya mlipuko.

Kwa upande wake, mtaalamu wa afya amesema mazingira yanapochafuka hujenga mazingira mazuri ya kuenea kwa magonjwa ya tumbo, huku maji yaliyotuama yakichochea kuzaliana kwa mbu wanaosababisha malaria.

Sauti ya kina Njau.