Dodoma FM

Wananchi Dodoma watakiwa kutunza vyanzo vya maji

19 May 2026, 17:47

Picha na meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Chamwino Silvia M. Ndimbo.Picha na Dodoma fm.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) ilianzishwa mwaka 2019 kupitia sheria ya maji  namba 5 ya mwaka 2019.

Na Elizabeth Tanzania.

Wananchi mkoani Dodoma wamesistizwa kutunza vyanzo vya maji vilivyopo, kutokana na uchache wa vyanzo hivyo, ili kuwezesha hali ya upatikanaji wa maji.

Akizungumza na taswira ya habari meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Chamwino Silvia M. Ndimbo amesema vyanzo vya upatikanaji wa maji wilayani chamwino hutegemea zaidi visima vya chini ya ardhi hivyo ni muhimu vikatunzwa kwa faida ya wananchi wote kwa ujumla.

Amesema kwa wilaya ya Chamwino hali ya upatikanani wa maji ni takribani asilia 77 huku asilimia 23 hawana huduma ya maji safi na salama ambapo vijiji 102 vinahudumiwa na RUWASA kati ya vijiji 107 vilivyopo, na vijiji 5 vinahudumiwa  na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa DODOMA     (DUWASA) huku kijiji kimoja kikikosa huduma hiyo ya maji.

Sauti ya Silvia M. Ndimbo.

Ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ipo miradi takribani 9 yenye thamani ya tsh Bilioni 4.2 ambayo ikikamilika kwa mwaka huu au ujao wa fedha itaongeza asilimia za upatikanaji ya maji kutoka asilimia 77 hadi asilimia 82.

Aidha amesema kwa kwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2026/2027 itahakikisha inakamilisha miradi ambayo bado haijakamilika na kuvipatia huduma ya maji vijiji ambavyo havina huduma hiyo.

Sauti ya Silvia M. Ndimbo.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) ilianzishwa mwaka 2019 kupitia sheria ya maji  namba 5 ya mwaka 2019, na kwa ngazi ya wilaya ikiwa na majukumu ya kuibua miradi ya maji, kusanifu miradi hiyo, kuijenga miradi mipya ya maji, kuunda na kusajili vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii, kudhibiti utendaji  wa vyombo hivyo na kuwajengea uwezo ili kutekeleza vizuri majukumu yao.