Wananchi walalamikia upimaji wa ardhi unaleta migogoro katika jamii
7 August 2026, 11:37

Kutokana na maelekezo ya mkuu wa wilaya wenyekiti wa mtaa wa Mbulu Mission Solomon Ruta amekiri kupokea maelekezo ya mkuu wa wilaya huku akiahidi kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Na Leokadia Andrew.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mbulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameeleza kutoridhishwa na shughuli za upimaji ardhi uliofanywa na idara ya ardhi. Wamesema upimaji wa ardhi umewaongezea migogoro kwenye maeneo yao kutokana na kufanyika bila kufuata utaratibu.
Wananchi wameeleza hayo katika mkutano wa hadhara ulioongozwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Frank Nkinda uliofanyika shule ya msingi Mbulu ambapo wananchi wameiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko yanayohusu usimamizi wa upimaji wa ardhi na kuhakikisha migogoro hiyo inatatuliwa kwa haki.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda awewataka wananchi kutoa taarifa za changamoto wanazokutana nazo hususan migogoro ya ardhi, huku akitaka viongozi wa mtaa kufanya mikutano ya mara kwa mara ili kubaini changamoto za wananchi zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.