Dodoma FM

Dodoma: Mtoto wa miaka 10 afariki kwa kujinyonga

9 September 2026, 16:25

Mtoto aliyemefariki mkoani dodoma dunia baada ya kujinyonga katika mazingira ambayo bado hayajaelezwa wazi. Picha na Anwary Shabani.

Tukio hilo limeacha simanzi kwa familia na wakazi wa Swaswa, huku likisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuwa na mawasiliano ya karibu na watoto wao na kuchukua hatua mapema wanapoona mabadiliko katika mwenendo au hali zao.

Na Anwary Shabani.

Mtoto mwenye umri wa miaka kumi, mkazi wa eneo la Swaswa jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kujinyonga katika mazingira ambayo bado hayajaelezwa wazi.

Akizungumza na vyombo vya habari, baba wa mtoto huyo, Saimon StanlayMzengo, amesema alipatwa na mshtuko baada ya kumkuta mwanawe akiwa amejifungia ndani ya chumba na tayari amefariki dunia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Swaswa, Hendrya Andrea, amesema wamepokea tukio hilo kwa masikitiko makubwa, huku akiwataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao, kuzungumza nao mara kwa mara na kufuatilia changamoto zinazowakabili.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Swaswa jijini Dodoma nao wameeleza kusikitishwa na tukio hilo, huku wakitoa wito kwa wazazi kuimarisha malezi na kuwaombea watoto wao ili kuwaepusha matukio yanayoweza kuhatarisha maisha yao.

Sauti na Anwary Shabani.