Dodoma FM

Lishe ni msingi muhimu wa afya na maendeleo ya mwanafunzi

29 September 2026, 17:23

Afisa Lishe Shirika la World Vision Tanzania Jane Mushi akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe.Picha na Mzalendo blog.

Mwanafunzi anayepata lishe bora huwa na nafasi nzuri ya kuwa makini na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kujifunza.

Na Daniel Njau.

Inaelezwa kuwa lishe bora ni msingi muhimu wa afya na maendeleo ya mwanafunzi, kwani humsaidia kuwa na nguvu, umakini na uwezo mzuri wa kujifunza.

Wataalamu wa afya na elimu wanasisitiza kuwa ulaji wa vyakula vyenye virutubisho muhimu unaweza kuboresha utendaji wa wanafunzi darasani na kuchangia mafanikio yao kitaaluma.

Wananchi wanasema kuna umuhimu kwa wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata mazingira bora ya kujifunzia, ikiwemo chakula chenye lishe, ili kuwasaidia kujenga afya njema na kupata nguvu wanapokuwa katika masomo.

Mshauri na mwalimu wa masomo ya malezi, Bi. Amina Ramadhani, anasema lishe bora kwa mwanafunzi ni muhimu katika kuongeza uelewa na kusaidia kuboresha ufaulu wake anapokuwa darasani.

Amesema mwanafunzi anayepata lishe bora huwa na nafasi nzuri ya kuwa makini na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kujifunza.

Ripoti ya Daniel Njau.