Dodoma FM

Asili ya jina la Bumira, historia ya Wabena yafichuliwa

28 October 2026, 18:00

Picha ni mbena akiwa amevaa nguo na kujipamba kiutamaduni. Picha na RFI.

Na Stephen Noel.

Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ina historia ya makabila mbalimbali yaliyoishi pamoja kwa muda mrefu, yakiwemo Wagogo, Wabena, Wakaguru na Wahehe. Mwingiliano wa makabila hayo umechangia kujenga urithi wa kihistoria na kitamaduni unaotambulisha eneo hilo.

Katika Kijiji cha Bumira, historia ya uwepo wa Wabena na asili ya jina la kijiji hicho imeendelea kuwa sehemu ya simulizi za wazee wa eneo hilo. Mzee George Kauya, mkazi wa kijiji hicho, anasema jina la Bumira lina asili ya lugha ya Kibena na linahusishwa na historia ya mababu waliohamia eneo hilo kutoka Njombe na maeneo mengine ya Kusini mwa Tanzania.

Kwa simulizi zaidi tuungane na Msimilizi wetu Na Stephen Noel.