Teknolojia yatajwa kuwa nyenzo muhimu ya kurahisisha shughuli
28 October 2026, 17:30

Jamii imetakiwa kuendelea kutumia teknolojia kwa uwajibikaji na kuzingatia usahihi wa taarifa inazopata, ili iweze kunufaika na maendeleo ya teknolojia katika elimu, mawasiliano na shughuli nyingine za kila siku bila kuathiri usalama na ustawi wake.
Na Daniel Njau.
Matumizi sahihi ya teknolojia yametajwa kuwa nyenzo muhimu katika kurahisisha majukumu ya kila siku, kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuboresha mawasiliano, huku wananchi wakihimizwa kuitumia kwa manufaa katika shughuli za kijamii, kielimu na kiuchumi.
Baadhi ya wananchi wamesema teknolojia imekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi katika kutafuta maarifa na kujifunza, huku ikirahisisha mawasiliano kati ya ndugu, jamaa na marafiki bila kujali umbali uliopo kati yao.
Kwa upande wake, mtaalamu wa masuala ya teknolojia, Bw. Jumanne mtabalike, amesema teknolojia inaweza kurahisisha shughuli nyingi za kila siku, ikiwemo upatikanaji wa taarifa za afya kupitia simu za mkononi.
Amesisitiza umuhimu wa kuitumia kwa usahihi na kuchagua taarifa kutoka vyanzo vinavyoaminika ili kuongeza manufaa yake katika maisha ya kila siku.