Dodoma FM

Walimu watakiwa kuwalinda watoto na ukatili maeneo ya shule

3 September 2026, 16:20

Walimu wametakiwa kuhakikisha wanasimamia elimu na usalama wa watoto katika shule zao.Picha na Dodoma fm.

Ametumia fursa hiyo kuwasihi walimu kuhakikisha wanasimamia elimu na usalama wa watoto katika shule zao.

Na Stephen Noel.
Walimu wameshauriwa kuwalinda watoto ili kuepuka vitendo vya ukatili vinavyoweza kujitokeza katika maeneo ya shule.

Wito huo umetolewa na baadhi ya wakuu wa shule walipokuwa wakizungumza na Dodoma FM wakati wa kikao cha wakuu wa shule kilicholenga kutathmini utendaji wao wa kazi kwa mwaka.

Grace, Mwenyekiti wa Wakuu wa Shule Mkoa wa Dodoma, amesema kwa sasa Dodoma inatazamwa na ulimwengu mzima katika nyanja mbalimbali, hivyo bila kuweka misingi imara ya elimu, maendeleo yanaweza kuchelewa.

Sauti ya Stephen Noel.