Dodoma FM

Maafisa usafirishaji(Bodaboda) waonywa kuacha kujihusisha na uhalifu

20 August 2026, 16:21

Picha ni maafisa usafirishaji , OCD na baadhi ya Askari katika picha ya pamoja baada ya kikao.Picha na Grace Budodi.

Aidha Maafisa usafirishaji wameelekeza lawama hizo kwa bodaboda ambao wamekuwa wakiingia vituo ambavyo si vyao na kufanya kazi hasa nyakati za usiku na kujikuta wakichafua jina la kijiwe hicho kwa kujikuta wakibeba wahalifu.

Na Grace Budodi.

Maafisa usafirishaji almaarufu kama Bodaboda wa kata ya Miyuji Jijini Dodoma wametakiwa kuacha kuruhusu  vyombo  vyao vya usafiri kutumika katika vitendo vya uhalifu.

Wito huo umetolewa na mkuu wa kituo wilaya OCD Daudi Nkuba alipokuwa akizungumza na maafisa usafirishaji wa kata ya Miyuji amesema Vyombo vya usafiri mara nyingi vimekuwa vikitumika katika vitendo mbalimbali vya uhalifu ikiwemo wizi na ubakaji hasa nyakati za usiku.

Akizungumza katika kikao na maafisa hao, OCD Daudi Nkuba amesema maafisa usafirishaji(bodaboda) kwa sasa wanatumika katika baadhi ya matukio ya uhalifu, hivyo amewataka kuwa makini na watu wanaowasafirisha pamoja na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa jamii.

Baada ya kikao hiki kutamatika Napata kiu ya kufahamu zaidi kutoka kwa maafisa usafirishaji almaarufu kama bodaboda  kutoka kwao nataka kufahamu je ni kwanini wamekuwa akihusishwa katika vitendo hivi na hapa wanajibu.

Sauti ya Grace kina.