Dodoma FM

Mlebe waiomba serikali kukarabati barabara

28 September 2023, 9:44 pm

Picha ni Barabara hiyo inayopita katika Kijiji hicho cha Mlebe .Picha na Mindi Joseph.

Ubovu wa miundombinu ya barabara umekuwa ukikwamisha shughuli za uchumi kwa wananchi kwani wanashindwa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Na Mindi Joseph.

Wananchi wa Kijiji cha Mlebe Wilayani Chamwino wameiomba serikali kuwakarabatia barabara inyaounganisha kijiji hicho na Mjini ili kuondoa adha wanayoipata kwa sasa.

Barabara hiyo ilifanyiwa ukarabati mwaka jana lakini hadi sasa imeshaharibika tena.

Baadhi ya wananchi wanasema ajali za mara kwa mara zimekuwa zikitokea

Sauti za wananchi.
Picha ni muonekano wa Barabara hiyo ya Mlebe. Picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Mpilimi  amesema tayari mbunge ameshachakua hatua na hivi karibuni ukarabati utaanza.

Sauti ya Bw. Joseph Mpilimi.