Tufikie Malengo ya 95-95-95 Kutokomeza maambukizi mapya ya UKIMWI
2 July 2026, 16:53

Mapambano dhidi ya UKIMWI ni suala mtambuka linalohitaji ushiriki wa kila idara.
Na Stephen Noel.
Jamii Wilaya ya Mpwapwa imetakiwa kuongeza juhudi katika kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na kuhakikisha watu wote waliogundulika wanaishi na virusi wanatumia dawa za ARV bila kukatiza.
Wito huo umetolewa na Dkt. Kikoti Mrijo, Mratibu wa Masuala ya UKIMWI, ugonjwa wa ini na Magonjwa ya Zinaa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dkt. Mrijo amesema Wizara ya Afya inalenga kufikia malengo ya kimataifa ya 95-95-95 ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini, Mhe. George Fuime, amesema elimu kuhusu UKIMWI inatakiwa kuendelea kutolewa kwa jamii kwa sababu sasa imepungua ikilinganishwa na awali.
Hata hivyo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Mpwapwa, Mhandisi Emanuel Lukumay, amebainisha kuwa mapambano dhidi ya UKIMWI ni suala mtambuka linalohitaji ushiriki wa kila idara.