Mradi wa AHADI kuwasaidia vijana kupata ujuzi
26 May 2026, 16:58

Mradi huo wa AHADI kwani utawasaidia vijana kupata ujuzi na kujiajiri ili kujiingizia kipato.
Na Victor Chigwada.
Vijana wa mtaa wa Ihumwa A jijini Dodoma wametakiwa kuchangamkia fursa zinazo telewa na mradi wa AHADI mtaani hapo ikiwemo mafunzo ya ufundi wa kushona .
Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo wa Kata ya Ihumwa Bi.Anna Masijita alipokuwa akiongea na taswira ya habari ambapo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi uandikishaji utakapo anza ili waweze kunufaika na mafunzo hayo.
Aidha Masijita amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa bure kwa vijana wote watakao jiandikisha hivyo ni vema kila kijana anae hitaji ashiriki mafunzo hayo.
Nao baadhi ya wakazi wa mtaa wa Ihumwa A wameshukuru kuletewa mradi huo wa AHADI kwani utawasaidia vijana kupata ujuzi na kujiajiri ili kujiingizia kipato.