Unywaji wa pombe kupita kiasi ni kikwazo cha maendeleo
12 August 2026, 17:18

Matumizi ya pombe kwa kiasi yanaweza kuepusha madhara kwa mtu, familia na jamii, huku akiwataka wananchi kuweka kipaumbele katika kujenga maisha yenye tija na kuwajibika kwa familia zao.
Na Daniel Njau.
Unywaji wa pombe kupindukia umetajwa kuwa miongoni mwa vikwazo vinavyoweza kumzuia mtu kufikia maendeleo binafsi na kifamilia, kutokana na muda na fedha nyingi kutumika katika pombe badala ya shughuli za maendeleo.
Baadhi ya wananchi wamesema wapo watu katika jamii wanaoshindwa kuthamini familia na kujithamini wenyewe kutokana na matumizi makubwa ya pombe. Hata hivyo, wengine wameeleza kuwa pombe si sababu pekee inayozuia maendeleo, bali ni sehemu ya starehe inayopaswa kutumiwa kwa kiasi.
Mshauri wa masuala ya familia na uchumi Bi Magdalena Mtei amesema mtu anayelewa kupindukia mara kwa mara hupoteza uwezo wa kupanga na kutekeleza majukumu yake ipasavyo, hivyo amemshauri kupunguza au kuacha kabisa matumizi hayo ili kuelekeza nguvu na kipato katika shughuli za maendeleo.