Wananchi Mpwapwa watakiwa kutumia kituo cha TEWW kujiongezea maarifa
18 May 2026, 13:59

Baadhi wa wanufaika wa mpango huo wamesema Jamii inatamani kukutumia sana kituo hicho lakini upungufu wa vifaa unasababisha watu kuto jitokeza .
Na Steven Noel.
Wananchi wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma wameshauriwa kukutumia kituo cha maarifa cha Elimu ya watu wazima Ili kujiongezea maarifa mtambuka Katika shughuli zao .
Kauli hiyo imetolewa na Matheo Mwita mratibu miradi kutoka shirika la DVV International alipokuwa akiongea Katika kikao kazi cha kujadili namna kituo cha Elimu ya watu wazima kinavyo weza kuwanufaisha wakazi hao .
Amesema kwa kushirikiana na serikali kupitia mpango wake wa MUKEJA( Mpango wa uwiano Kwa Jamii) shirika Hilo wameamua kuanzisha vituo vya ujifunzaji Kwa Jamii ambapo Jamii itajiongezea maarifa mbalimbali kama kilimo,ufugaji wa Kuku,utunzaji wa familia na lishe.
Kwa upande wake Afisa Elimu watu wazima wilayani hapa bwana Yohana Myovela amesema Jamii ikiamua kutumia kituo hicho Kwa tija wanaopata manufaa makubwa Katika masuala mtambuka .