Dodoma FM
Dodoma FM
28 April 2026, 15:33

Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kilimo kwa kuweka mindombinu ya kisasa hususani katika kilimo cha umwagililiaji.
Na Victor Chigwada.
Vijana wametakiwa kujikita kwenye fursa mbalimbali ili kujiingizia kipato na kuacha kisingizio cha kukosa ajira .
Wakiongea na taswira ya habari baadhi ya vijana wamesema vijana wengi wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii pasipo kubuni njia za kujiingizia kipato au kuitumia mitandao hiyohiyo ya kijamii kujiingizia kipato.
Ngw’ashi Muhuri afisa maendeleo Kata ya Msamalo amesema kuwa dhana potofu ya vijana kuamini watu wa vijijini ndio wanahusika na kilimo ndio imewafanya vijana wengi kuendelea kulalamikia ukosefu wa ajira .
Aidha amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kilimo kwa kuweka mindombinu ya kisasa hususani katika kilimo cha umwagililiaji hivyo vijana wanapaswa kuiona fursa ya kilimo na kuitumia kujikwamua kimaisha.