Dodoma FM

NEMC yaanza oparesheni kudhibiti vifungashio visivyo takiwa

18 April 2023, 6:06 pm

Vifungashio visivyo takiwa kupigwa marufuku. Picha na Fred Cheti.

Mnamo tarehe 1 Juni, 2019, Serikali ilipiga Marufuku Uzalishaji; Uingizaji nchini, Usafirishaji nje ya nchi; Usambazaji; na Matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kile kinachodaiwa kuwa mifuko hiyo ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira.

Na Fred Cheti.

Serikali kupitia baraza la usimamizi na uhifadhi mazingira NEMC imeanza opresheni maaalumu ya kutembelea na kukagua masoko mbalimbali nchini kwa ajili ya kudhibiti vifungashio visivyotakiwa.

Opresheni hiyo imeanza jijini Dar es salaam ambapo inatarajia kufanyika katika masoko yote nchini na katika opresheni hiyo jumla Magunia 50 ya vifungashio vilivyopigwa marufuku vimekamatawa katika masoko ya Kisutu na Machinga Complex Centre kama anavyobainsha Afisa mazingira mkuu wa baraza hilo Bi. Flora Akwilapo.

Sauti ya Afisa mazingira mkuu

Aidha Bi Flora amewataka wafanyabiashara pamoja na wanachi wote nchini kuepuka kuingia katika mgogoro na serikali kwa kufuata utaratibu wa kutumia vifungashio vilivyoruhusiwa na serikali.

Sauti ya Afisa mazingira mkuu