Dodoma FM

Wanafunzi watakiwa kutofumbia macho vitendo vya rushwa

13 November 2023, 4:07 pm

Picha ni wanafunzi kutoka Shule 12 ambazo ziliingia fainali katika  shindano la Mdahalo wa Shule za Sekondari Dodoma .Picha na Seleman Kodima.

Na Seleman Kodima.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabiri Shekimweri  amewataka wanafunzi wa Shule za Sekondari Dodoma kupinga, kuchukia na kutofumbia matendo ya rushwa.

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na shule 12 ambazo ziliingia fainali katika  shindano la Mdahalo wa Shule za Sekondari Dodoma lililoandaliwa kwa ushirikiano wa mkuu wa wilaya ya Dodoma na  Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa mkoa wa Dodoma lengo likiwa ni   kuwajengea wanafunzi uwezo na ari ya kujiamini na kupambana na vitendo vya rushwa, kujieleza, kujenga hoja, kuhoji na zaidi kuwajengea uwezo wa maarifa na kitaaluma.

Alhaji Shekimweri amewaasa wanafunzi hao kuhakikisha wanakataa aina yeyote ya Vitendo vya Rushwa .

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabiri Shekimweri.
Picha ni Baadhi ya wanafunzi walio shiriki katika mkutano huo. Picha na Seleman Kodima.

Aidha amewataka wanafunzi hao kuwa mstari wa Mbele kutoa Elimu kwa wazazi na walezi wao kuhusu Rushwa na kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kupinga Vitendo hivyo .

Mkuu huyo wa wilaya amesema amepokea mapendekezo ya ushirikishwaji wa wanafunzi wa shule za Msingi katika mashindano hayo ili kuweze kutoa nafasi ya wanafunzi wote kujengewa uwezo wa mapambano dhidi ya Rushwa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabiri Shekimweri.

Awali akisoma Risala kuhusu Mshindano hayo ,Mjumbe wa Sekretarieti  ya mashindano hayo Mwl Salim Dewji amesema kuwa kupitia mashindano hayo wamefanikiwa kufikisha Elimu ya kupinga vitendo vya Rushwa kwa wanafunzi laki moja .

Sauti ya Mwl Salim Dewji .
Picha ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma akitoa vyeti vya pongezi kwaajili ya ushiriki. Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wake Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa mkoa wa Dodoma Amewataka washirikishi wa mdahalo huo kutambua wajibu wao wa kupambana na rushwa katika utoaji wa taarifa kwa Mamlaka zinazoshughulikia jinai.

Sauti ya Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa mkoa wa Dodoma

Huu ni Mwaka wa Pili tangu kuanzishwa kwa Mashindano hayo ambayo muasisi wake ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma ambapo Mwaka huu mashindano hayo yamehusisha shule 60 za Sekondari Dodoma na Kushuhudia shule ya Sekondari Bunge wasichana wakiwa mabingwa kwa mwaka 2023 na kuzawadia Compture mpakato na Kiasi cha Shilingi laki moja Taslimu.