Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuweka tamaduni ya kuzungumza na vijana juu ya afya ya uzazi

5 November 2021, 1:26 pm

Na; Mariam Matundu.

Jamii imeshauriwa kuacha tamaduni za kutozungumza na watoto wao na badala yake wawe wa wazi katika kufikisha elimu ya afya ya uzazi.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya vijana wamesema kuwa wanakumbwa na sintofahamu juu ya afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu juu ya matumizi ya uzazi wa mpango.

Nae daktari Chesko Muhema kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kitengo cha magonjwa ya mama na mtoto amesema ni muhimu vijana kupewa elimu hii kulingana na umri wake kwa kuwa afya ya uzazi ni sehemu ya maisha.

Aidha amesema hakuna madhara yoyote ya kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango isipokuwa ni maudhi madogodogo yanayotofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Utafiti wa shirika la afya ulimwenguni WHO umebaini kuwa theluthi mbili ya wanawake wenye uwezo wa kubeba mimba na amabao wanania ya kuchelewa kupata ujauzito au kudhibiti idadi ya watoto huacha kutumia huduma za uzazi wa mpango kwa hofu ya madhara ya huduma hizo .