Dodoma FM

Umbali mrefu chanzo wanafunzi kukatisha masomo Mbandee

30 October 2023, 12:20 pm

Mradi wa BOOST umeendelea kuimarisha elimu msingi na kwani takribani shilingi trilioni moja zimejenga madarasa ya shule za msingi 9,705.

Kupitia mradi wa BOOST umeendelea kuimarisha elimu msingi kwani takribani shilingi trilioni moja zimejenga madarasa ya shule za msingi 9,705 na kukarabati shule za msingi kongwe kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Na Mindi Joseph.

Umbali mrefu wanaotembea wanafunzi wa kitongoji cha Mbandee kwenda kusoma shule ya Wiliko umetajwa kuwa kikwazo cha kuwakatisha tamaa na kushindwa kumaliza masomo.

Diwani wa Kata ya Mlowa Bwawani Andrew Mseya ameyabainisha hayo kupitia mahojiano na Dodoma Fm huku akilishukuru shirika la AFNET kwa mchango wake katika kutatua changamoto hiyo.

Sauti ya Andrew Mseya .

Mwakilishi wa shirika la AFNET anasema shirika hilo linatekeleza miradi ya elimu katika kata 4 ikiwemo kata ya Mlowa Bwawani huku akiwataja wananchi kuwa wamejitolea katika ujenzi wa maboma ya shule.

Sauti ya Mwakilishi wa shirika la AFNET.