EWURA CCC yaendelea kulinda na kutetea watumiaji huduma za nishati na maji
24 June 2026, 11:24

Eneo lingine lililopatiwa kipaumbele ni uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kufanikisha lengo la Taifa la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Watumiaji wa huduma za nishati na maji zaidi ya 500 wamefika katika barazala ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji(EWURA CCC) na kueleza kero zao pamoja na kupatiwa ufafanuzi pamoja na malalamiko hayo kufikishwa mamlaka husika.
Akiongea na waandishi wa habari katika kufunga wiki ya utumishi Afisa huduma kwa wateja kutoka Ewura ccc Bw. Amani Mbogo amesema wananchi wengi wanapitia chanagamoto za matumizi ya nishati na maji lakini hawajui kero hizo wanapaswa kuziwalisha wapi hivyo amewataka kulitambua baraza hilo na kuwasilisha kero hizo ili ziweze kufikishwa sehemu husika.
Bw. Mbogo amesema mamlaka hii ni muhimu kwa wananchi wote wanao tumia huduma za nishati na maji hivyo bado wanatamani kuwafikia watu wengi na kupokea kero na changamoto zao.
Aidha amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupima mitungi ya gesi wanaponunua katika maduka mbalimbali ili kuhakikisha wanapata ujazo sahihi wa gesi kulingana na kiwango kilichokusudiwa.
EWURA CCC inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda na kutetea watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji, kupokea malalamiko ya watumiaji na kuwaelekeza utaratibu wa utatuzi wake.
Aidha, EWURA CCC imekuwa ikifuatilia malalamiko hayo ili kuhakikisha yanatatuliwa kwa wakati na mamlaka husika kwa ustawi wa watumiaji na kufanya huduma ziwe bora na endelevu.