Dodoma FM

Bilioni 27 zatarajiwa kutumika ujenzi wa bwawa Chunyu

20 October 2022, 11:59 am

Na;Mindi Joseph.

Bilioni 27 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa bwawa la umwagiliaji katika kijiji cha chunyu wilayani mpwawa ili kutatua changamoto ya uzalishaji hafifu wa Chakula.

Hivi karibuni wanachi wa kijiji hicho wameelezea kuwa ukosefu wa Bwawa na Skimu za umwagiliaji  imechangia uzalishaji hafifu na kusabaisha kushindwa kujikwamua kiuchumi.

Taswira ya Habari imezungumza na Mhandisi wa Umwagilija Mkoa wa Dodoma Raphael Laizer  ili kufahamu ujenzi wa Bwawa hilo .

.

Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga bwawa hilo Emmanuel Mponda amesema ujenzi wa Bwawa hilo utawanufaisha wananchi wa eneo hilo katika kilimo cha umwagiliaji.

.

Ujenzi wa bwana hilo utawanufaisha zaidi wananchi wa kata ya Ngh”ambi na Chunyu na unatarajiwa kukamilika baada ya  miezi 18