Dodoma FM

Viongozi wa kijiji Zejele watakiwa kuacha kujihusisha na uuzaji wa maeneo

21 July 2023, 4:11 pm

Mbunge wa Bahi Mh. Kenneth Nollo akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa kijiji cha Zejele.Picha na Seleman Kodima.

Mhe Nolo amesema kuwa  serikali ya kijiji isijiingize kwenye udalali wa kuuza ardhi kwani itakuwa ni chanzo cha mgogoro kwa wananchi .

Na Seleman Kodima.

Viongozi wa serikali ya kijiji cha Zejele kata ya Nondwa wametakiwa kuacha  kujihusisha na uuzaji wa maeneo ili kuepukana na migogoro ya ardhi.

Wito huo umetolewa na mbunge wa Bahi Mhe. Keneth Nolo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji zejele katika mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa Bahi.

Sauti ya mbunge wa Bahi.

Aidha amewataka viongozi wa serikali ya kijiji kuwatetea wananchi maana wana wajibu wa kuwatumikia wananchi ambao wamewapa mamlaka ya kuwaongoza.

Wananchi wa Kijiji cha Zejele wilayani Bahi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo. Picha na Seleman Kodima.

Wakati huohuo amezungumzia mpango wa serikali wa ujenzi barabara  ya  Bihawana, Chali, Chifutuka  hadi Sanza Manyoni kwa  kiwango cha lami na kuwahakikishia wananchi wa Zejele kujiandaa kwa ajili fursa ya uwepo wa barabara hiyo katika kujiletea maendeleo yao.

Sauti ya Mbunge wa Bahi.