Dodoma FM

Vilio vyatanda wajasiriamali Dodoma

18 March 2021, 10:42 am

Na, Shani Nicholous.

Wajasiriamali jijini Dodoma wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt.John Pombe Magufuli.

Wakizungumza na taswira ya habari wajasiriamali hao wamesema kuwa watamkumbuka kwa mengi aliyowatendea kwani chini ya uongozi wake unyanyasaji kwa wafanyabiashara ulikomeshwa huku akiwatetea kwa mengi hali iliyowafanya kuendesha biashra zao vizuri.

Aidha wamempongeza na kumshukuru kwa yale yote aliyoyafanya kwa kipindi chote cha uhai wake kwa kuwa ameacha alama kubwa kwao huku wakiahidi kuishi katika misingi na hekima walizoachiwa na kiongozi huyo.

Hayati Rais Dkt.John Pombe Magufuli alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 na amefariki Machi 17 mwaka 2021. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, amen.