Dodoma FM

Viongozi wapya walio apishwa watakiwa kufanya kazi kwa bidii

11 January 2022, 2:35 pm

Na; Thadei Tesha.

Wananchi jijini Dodoma wamewaomba viongozi wapya walioapishwa kufanya Kazi kwa bidii kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi jijini hapa wamesema viongozi hao wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanafanya Kazi kwa bidii ili kuendana na Kasi ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha baadhi ya wananchi wamemshukuru rais wa jamhuri ya muungano waTanzania Mh Samia suluhu Hasan kwa Kazi nzuri ya kuibua na kujenga miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa Nchini kote.

Prf.Adolf mkenda ni miongoni mwa mawaziri walioteuliwa kuwa waziri wa elimu kutoka wizara ya kilimo ya hapo awali Amesema ataendelea kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha anawaletea wananchi maendeleo Kama alivyokusudia mh rais.

Waziri mkenda aliyasema hayo wakati akikabidhiwa ofisi ya wizara ya elimu iliyopo mji wa kiserikali mtumba jijini hapa.