Dodoma FM

Wanafunzi 180 wa kidato cha tano hawajaripoti shuleni Msalato

27 September 2023, 5:42 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule akiwa shule ya sekondari Msalato.Picha na Yussuph Hassan.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametembela Jumla ya Miradi Mitatu inayoendelea Jijini Dodoma ikiwemo Ujenzi wa Mabweni Mawili ya Shule ya Sekondari Msalato, Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika Kata ya Nala na Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mpamaa kata ya Miyuji.

Na Yussuph Hassan.

Wanafunzi wapatao 180 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya Sekondari Wasichana ya Msalato hawajaripoti shuleni hapo kati ya Wanafunzi 460 waliochaguliwa.

Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule katika kukagua miradi ya maendeleo amepita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato na kutoa agizo hili.

Sauti ya Mh . Rosemery Senyamule.
Picha ni ujenzi wa mabweni na madarasa unaoendelea . Picha na Yussuph Hassan.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri anaeleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana ya Msalato.

Sauti ya Mh. Jabir Shekimweri.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alitembelea ujenzi wa Hospital ya Dodoma inayojengwa katika eneo la Nala.

Risala.