Dodoma FM

Wananchi waishukuru serikali kwa kusaidia ujenzi wa kituo cha afya

8 March 2023, 1:40 pm

Wananchi wa Kata ya Itiso Wilaya ya Chamwino.Picha na wikipedia

Wananchi wa Kata ya Itiso Wilaya ya Chamwino wameishukuru Serikali kwa jitihada za kuboresha huduma za afya kwa kuwasaidia ujenzi.

Na Victor chigwada.

Wananchi wa Kata ya Itiso Wilaya ya Chamwino wameishukuru Serikali kwa jitihada za kuboresha huduma za afya kwa kuwasaidia ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo cha afya.

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti na Taswira ya habari wananchi hao wamesema kuwa pamoja na ujenzi huo wa kituo cha afya ambacho bado hakijaanza kutumika ni vyema Serikali kuongeza upatikanaji wa dawa katika zahanati na vituo vya afya.

Sauti za wananchi.

Diwani wa Kata ya Itiso Bw. Simoni Matambila amesema kwasasa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kabla ya kukifungua ili kianze kazi rasmi.

Aidha ameongeza kuwa changamoto nyingine ni suala la bima ya afya kwani wananchi walio jisajili na bima ya afya wamekuwa hawapati huduma kikamilifu hali inayowakatisha tamaa baadhi ya wananchi wanaotaka kujiunga na mfuko huo wa Bima ya afya.