Dodoma FM

Chipogolo walazimika kufuata baadhi ya huduma za Afya Mtera

29 February 2024, 3:48 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa pamoja na wajumbe wengine wakikagua kituo hicho cha Afya. Picha na Yussuph Hassan.

Mh. Senyamule ametembelea kituo cha afya cha Rudi ambacho kinahudumia wananchi takribani 15,440 kutoka vijiji vitano, kituo kilipokea kiasi cha shilingi Milioni 701 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara ambayo ipo katika hatua ya umaliziaji na Shilingi Milioni 300 kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha Afya cha Chipogolo kwenye Jengo la upasuaji, wodi ya wazazi na Maabara.

Na Mariam Kasawa.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma ametoamaagizo kukamilika haraka kwa kituo cha Afya cha Chipogolo wilaya Mpwapwa.

Kituo cha Afya Chipogolo kimekamilika kwa kiasi kidogo huku baadhi ya majengo yakiwa bado kama jengo la upasuaji hali inayo walazimu wananchi kufuata huduma katika hospitali ya Mtera.

Amesema baadhi ya huduma zimeanza kutolewa kituoni hapo lakini baadhi ya majengo hayajakamilika hivyo anahitaji ukamilishaji wa haraka.

Sauti ya Mh. Rosemery Senyamule.
Picha ni Mkazi wa Chipogolo akieleza changamoto za kijijini hapo kwa Mkuu wa Mkoa. Picha na Yussuph Hassan.

Katika mkutano huo na wananchi mkuu wa mkoa aliwapa nafasi wakazi wa Chipogolo kueleza changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo kijijini hapo.

Sauti za baadhi ya wananchi.