Dodoma FM

Miundombinu bora ni chachu ya ufaulu katika shule za umma

31 March 2021, 11:43 am

Na; Mindi Joseph

Imeelezwa kuwa uboreshaji wa miundombinu na usimamizi makini unahitajika kwa shule za Umma ili kuongeza morali ya kufanya vizuri kwa wanafunzi Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa matokeo ya Baraza la Mitihani Tanzania NECTA kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 yanaonyesha shule mbili za Serikali ndizo zilizofanikiwa kuingia kwenye Shule kumi Bora za Mkoa huku binafsi zikiwa nane.

Taswira ya habari imezungumza na   baadhi ya walimu  Mkoani Dodoma ambapo wamebainisha kuwa Shule za Serikali hazifanya vizuri kutokana na changamoto ya miundombinu kwani shule za binafsi zinamiundombinu rafiki.

Katika hatua nyingine Taswira ya Habari imezungumza na Mhadhiri kutoka chuo cha DUSE Dar es salaam, Dk Luka Mkonongwa na amesema ili  shule za serikali ziweze kufanya vizuri  usimamizi makini unahitajika pamoja na uboreshaji wa miundombinu.

Shule za Sekondari Msalato na Mpwapwa hazijawahi kutoka katika 10 bora kimkoa kati ya shule zaidi ya 290 za Mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta)