Dodoma FM

Watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa kuhujumu miundombinu ya reli

11 April 2024, 4:59 pm

Wananchi wameaswa kujiepusha na vitendo vya kuhujumu reli. Picha na Google.

Vitendo vya uhujumu wa miundombinu ya umeme vinakwamisha jitihada za Serikali za kutoa huduma ya uhakika ya umeme kwa wananchi.

Na Fred Cheti.
Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za kuhujumu miundombinu ya shirika la umeme Nchini (Tanesco) Mkoani Dodoma.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe Jabir Shekimweri ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Dodoma amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kuwatahadharisha wananchi kujiepusha na vitendo hivyo.

Amesema vitendo vya uhujumu wa miundombinu ya umeme vinakwamisha jitihada za Serikali za kutoa huduma ya uhakika ya umeme kwa wananchi huku akiahidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika tukio hilo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe Jabir Shekimweri.

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma Mhandisi Donasiano Shamba amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika mamlaka husika pindi wanapobaini uharibifu au wizi wote katika miundombinu ya shirika la umeme Tanzania Tanesco.