Dodoma FM

Asasi za kiraia mpwapwa za chukizwa na kasi ya uharibifu wa mazingira

3 August 2026, 17:26

Asasi za kiraia zimekuwa chachu ya kuchochea maendeleo kufuatia afua mbalimbali wilayani mpwapwa. Picha na Stephen Noel

“Fikira Mpya, Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Ubunifu, Ubia na Upatikanaji wa Rasilimali Fedha Kupitia Vyanzo vya Ndani.

Na Stephen Noel.

Serikali ya Wilaya ya Mpwapwa imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuchochea utekelezaji wa kasi na kufikia malengo ya taifa ya mwaka 2050.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, ambaye pia ni Katibu Tawala wa Tarafa ya Mpwapwa, Bwana Obert Mwalyego alipokuwa akifungua Jukwaa la Asasi za Kiraia lililofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya.

Mwalyego amesema asasi za kiraia zimekuwa chachu ya kuchochea maendeleo kufuatia afua mbalimbali zinazotekelezwa na asasi hizo wilayani hapa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bwana Bahati Magula amesema Mpwapwa ina mashirika 24 yanayofanya kazi katika idara mbalimbali.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa asasi hizo akiwemo Emanuel Majele kutoka Shirika la Lead Foundation wameelezea kuwa na wasiwasi na kasi ya uharibifu wa mazingira wilayani hapo.

“Tunakereka na kasi ya uharibifu wa mazingira. Hali hii inarudisha nyuma jitihada za wadau wa mazingira” amesema Majele.

Jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Mpwapwa la mwaka 2026 limekuwa na kauli mbiu isemayo.

Sauti na Stephen Noel.