Matumizi ya vilevi waathiri masomo kwa wanafunzi
10 September 2026, 16:58

Wananchi jijini Dodoma wameelezwa umuhimu wa elimu ya afya na malezi bora kama hatua zinazoweza kusaidia kuwalinda vijana dhidi ya madhara ya matumizi ya vilevi na kuwawezesha kuzingatia masomo yao.
Na Crispine Gerald.
Matumizi ya vilevi kama pombe na dawa za kulevya yametajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kuathiri afya, tabia, masomo na maendeleo ya vijana, huku wanafunzi wakielezwa kuwa katika hatari ya kushuka kwa ufaulu na utendaji wao wa kitaaluma.
Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya vijana jijini Dodoma ili kufahamu uelewa wao kuhusu madhara ya vilevi kwa wanafunzi, ambapo wamesema matumizi ya vilevi yanaweza kusababisha kushuka kwa ushiriki darasani, ufaulu mdogo na hata baadhi ya wanafunzi kuacha shule.
Akizungumzia suala hilo, Mwalimu Mshamu Abdalla amesema matumizi ya vilevi yanaweza kuathiri uwezo wa mwanafunzi kuzingatia masomo, kuhudhuria vipindi na kutimiza majukumu yake ya kitaaluma.