Ujasiriamali watajwa kuwa fursa ya jamii kujiajiri
11 September 2026, 16:05

Watu wenye uelewa na uzoefu katika ujasiriamali wanapaswa kuendelea kutoa elimu na kuwatia moyo wengine, hususan vijana, ili waweze kuanzisha shughuli za kuwaingizia kipato na kujikwamua kiuchumi badala ya kusubiri ajira rasmi.
Na Daniel Njau.
Ujasiriamali umetajwa kuwa miongoni mwa njia muhimu za kujiajiri na kuongeza kipato, hasa kwa vijana wanaokabiliwa na changamoto ya ajira, huku elimu na uelewa wa fursa za ujasiriamali zikihitajika kuimarishwa katika jamii.
Pamoja na umuhimu wake, Baadhi ya wananchi wanasema elimu ya ujasiriamali bado haijawafikia watu wengi, hali inayofanya baadhi ya vijana kushindwa kutambua fursa zilizopo na namna ya kuzitumia katika kujikwamua kiuchumi.
Elimu hiyo inaweza pia kupatikana nje ya mfumo rasmi wa darasani na kumsaidia mtu kuanzisha shughuli kulingana na uwezo na mazingira yake.
Mkufunzi wa masomo ya ujasiriamali na mjasiriamali, Bi. Alisia Kasunga, amesema ujasiriamali ni shughuli ya mtu kujiajiri kwa lengo la kufikia malengo ya kiuchumi, ingawa baadhi ya watu bado wanakabiliwa na changamoto za kutambua umuhimu na manufaa ya ujasiriamali.