Dodoma FM

Usomaji wa vitabu wazidi kusahaulika katika jamii

28 August 2026, 17:09

Vitabu vimeendelea kuwa chanzo muhimu cha elimu na maarifa mbalimbali. Picha na mtandao.

Baadhi ya watu wanasema maendeleo ya teknolojia yamerahisisha upatikanaji wa taarifa na maarifa mtandaoni, hivyo hawaoni umuhimu wa kutumia muda mwingi kusoma vitabu.

Na Daniel Njau.

Usomaji wa vitabu unaonekana kupungua katika jamii kutokana na kasi ya matumizi ya intaneti na mitandao ya kijamii, hali inayotajwa kupunguza hamasa ya baadhi ya watu kujisomea vitabu kwa ajili ya kuongeza maarifa.

Baadhi ya watu wanasema maendeleo ya teknolojia yamerahisisha upatikanaji wa taarifa na maarifa mtandaoni, hivyo hawaoni umuhimu wa kutumia muda mwingi kusoma vitabu.

Hata hivyo, wengine wanaeleza kuwa vitabu vimeendelea kuwa chanzo muhimu cha elimu na maarifa mbalimbali yanayosaidia kujenga uelewa wa jamii.

Mwandishi wa vitabu mbalimbali, Iddy Mwalimu, amesema hali ya usomaji wa vitabu kwa sasa ni tofauti na ilivyokuwa hapo awali, kwani idadi ya watu wanaojisomea vitabu imepungua Huku watu wakiamini mitandao ya kijamii inakila kinancho hitajikankatika maisha ya kila siku.

Amesema baadhi ya watu wanaamini kuwa mitandao ya kijamii ina kila kitu, lakini wanasahau kuwa vitabu vina maarifa na mafundisho ya kina yanayoweza kusaidia katika kujenga jamii yenye uelewa na elimu.

Sauti na Daniel Njau.