

10 October 2024, 3:28 pm
Na Anwary Shabani
Utumaji wa nyaraka na usafirishaji wa vivurushi kupitia Shirika la Posta ni salama zaidi kulinganisha na njia zingine.
Wadau na watumiaji wa huduma za Posta wamebainisha hayo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa watumiaji bora wa huduma za posta pamoja na washindi wa shindano la uandishi katika kuadhimisha siku ya posta duniani na wiki ya huduma kwa mteja.
Katika maadhimisho hayo, Elton Thomson ambaye ni mwanafunzi ameibuka mshindi kwa kujishindia kitita cha pesa taslim kiasi cha Tsh 700,000/= (shilingi laki saba) katika shindano la uandishi .
Ufanisi wa utoaji wa huduma kwa shirika la posta kunatokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha shirika hilo kujiendesha na kutengeneza faida. Meneja wa shirika la posta Dodoma Bwn. Dongwe James Dongwe amepongeza na kushukuru kwa jitihada hizo.