Dodoma FM

Jamii imetakiwa kufichua mimba za utotoni ili kumkomboa mtoto wa kike

4 August 2021, 10:46 am

Na;Benard Filbert.

Young & Alive Initiative on Twitter: "TATIZO LA MIMBA ZA UTOTONI HUANZA NA  WAZAZI KUKOSA UJASIRI KUONGEA NA WATOTO WAO. #chagua #Beijing25tz… "

Jamii imeombwa kutokufumbia macho na badala yake kufichua vitendo vya mimba za utotoni ili kuepusha kumkosesha haki za msingi mtoto wa kike.

Wito huo umetolewa na afisa maendeleo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi Onalatha Rwegasira wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mkakati uliopo kutokomeza mimba za utotoni katika mkoa wa Dodoma.

Amesema mkakati uliopo ni kuhakikisha kila mmoja anakuwa na elimu juu ya athari za mimba za utotoni ikiwa ni pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa kuelimisha jamii kupitia kwa wadau mbalimbali mbalimbali ili kuifikia jamii.
Ameongeza kuwa Dodoma ni miongoni mwa mikoa yenye tatizo la mimba za utotoni hivyo juhudi za kila mmoja zinatakiwa kukomesha vitendo hivyo na sio kuitegemea serikali pekee.

Baadhi ya wazazi wameiambia taswira ya habari elimu inatakiwa kwa kiasi kikubwa kuanzia shuleni kwani baadhi yao watoto wa kike wamekuwa wakikutana na changamoto za mimba za utotoni hususani wakati wa kwenda shule kutokana na baadhi ya watu kutumia mwanya huo kuwalaghai.

Serikali imekuwa ikijitahidi kuzuia mimba za utotoni kwa kiasi kikubwa nchini kupitia kwa maafisa mbalimbali lengo ikiwa kila mtoto wa kike atimize ndoto zake ikiwemo ndoto ya kufika mbali kielimu kwani ni haki ya msingi.