Dodoma FM

Mapambano dhidi ya upungufu wa kuona unao epukika ifikapo 2030 yaendelea kufanyika

17 March 2023, 5:04 pm

Baadhi ya wadau wakiwa katika uzinduzi wa mradi wa afya ya macho. Picha na Mindi Joseph.

Kwa mujibu wa makadirio ya shirika la afya duniani WHO Sababu kubwa zikiwa ni mtoto wa jicho na shinikizo la macho.

Na Mindi Joseph.

Watu wenye matatizo ya kuona kwa kiwangao cha kati na cha juu hapa nchini wanakadiriwa kuwa ni mara tatu ya watu wasioona ikiwa ni takribani watu milion 1.86.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mpango wa Taifa wa huduma za Macho Dkt Bernadetha Shilio katika uzinduzi wa mradi wa afya ya macho amesema wanaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kutokomeza upungufu wa kuona unaoepukika ifikapo mwaka 2030.

Sauti ya Meneja wa Mpango wa Taifa wa huduma za Macho Dkt Bernadetha Shilio .

Kufuatia Changamoto hiyo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la (CBM) Tanzania Bi Nesia Mahenge amesema wametoa shilingi bilion 1.47 Kufadhili mradi wa afya ya macho.

Akiwasilisha taarifa kwa Mgeni rasmi Dr Ubuguyu alikuwa na haya yakusema.

Sauti ya Dr Ubuguyu.

Takwimu za Tanzania zinaonyesha kuwa watu Milioni 1347000 kwa mwaka 2022 walifikiwa na huduma ya macho katika vituo vya afya ikilinganishwa na uhitaji wa takribani watu milioni 12.