Dodoma FM

Matumizi ya pombe katika mikusanyika yachangia maambukizi ya uviko 19

20 September 2021, 11:54 am

Na; Shani Nicolous.

Imeelezwa kuwa matumizi ya pombe katika jumuiya na kwenye mikusanyiko yanachangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya uviko 19.

Akizingumza na Taswira ya habari Dr. Missan Yango kutoka hospitali ya Mkoa Dodoma amesema kuwa kutumia pombe sehemu za mikusanyiko ni ngumu kuzingatia njia ya kujikinga na Uviko 19 hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuzingatia ushauri wa taalamu wa afya juu ya matumizi bora ya pombe.

Amesema kuwa pombe ni chanzo cha kupata magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo husababisha kupata UVIKO-19 ambao utapelekea kupoteza maisha.

Ameongeza kuwa matumizi ya pombe kwa wakati mmoja na dawa ni hatari hivyo ni vema kuzingatia kuacha kutumia pombe pindi mtu akiamua kupata chanjo ili kuruhusu dawa hiyo kufanya kazi vizuri walau kwa wiki mbili kama mamlaka za afya zinavyoshauri.

Baadhi ya wananchi jijini Dodoma wameiambia Taswira ya habari kuwa matumizi ya pombe yamechukua nafasi kubwa katika jamii hasa pombe za kienyeji hivyo inahitajika nguvu kubwa kuelimisha juu ya matumizi sahihi na kiwango stahili cha pombe hizo.

Matumizi ya pombe kupita kiasi ni hatari hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Uviko 19 jamii inapaswa kuzingatia maagizo mbalimbali kutoka kwa serikali na wizara ya afya ili kuendeleza mapambano.