Dodoma FM

Wananchi Membe waomba semina zaidi mradi wa bwawa

13 September 2023, 5:46 pm

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema  wamekuwa na mkanganyiko kuhusu Mradi.Picha na Uhondo .

Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji unatarajia kuchukua takribani hekari 8000 ambapo ndani yake ndipo yanapatikana mashamba ya wananchi wanao hitaji kufahamu hatima ya mashamba hayo.

Na Victor Chigwada.

Uelewa wa wananchi wa Kijiji cha Membe wilayani chamwini kuhusu Mradi wa  bwawa la umwagiliaji linalotekelezwa kijijini hapo bado upo chini hali iliyowalizimu wananchi hao kuomba semina  zaidi

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema  wamekuwa na mkanganyiko kuhusu Mradi huo kutokana na kuachwa nyuma katika hali ya ushirikishwaji wa kila hatua ya utekelezwaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa hilo

Sauti za wananchi.

Aidha wamesema licha ya jitihada za kuendelea kufuatilia na kutaka kufahamishwa juu ya nini kinaendelea katika mradi huo lakini wameshindwa kupewa majibu ya kujitosheza kutoka kwa  viongozi wa kijiji hadi ngazi ya  Kata.

Sauti za wananchi.
baadhi ya mafundindi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa Bwawa la Membe Wilayani Chamwino.Picha na Michuzi blog.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa Chitabuli Kata ya Membe Bw.Keneth Msindwa amekiri wananchi wa kijiji chake na vijiji jirani wamekuwa na uhitaji wa majibu ya kutaka  kufahamu hatima ya mashamba yao yanayo twaliwa kwaajili ya mradi huo.

Sauti ya Kenneth Msindwa.

Msindwa amesema kuwa kukosekana kwa maelezo ya kutosha juu mradi huo imekuwa kero kwa wananchi na kuiomba Serikali kupitia Wizara husika kulitilia maanani jambo hilo.

Sauti ya Kenneth Msindwa.