Dodoma FM

Mwanafunzi afariki kwa kugongwa na gari katika kivuko

18 January 2024, 8:25 am

Picha ni waombilezaji wakiwa wamekusanyika kanisani kwaajili ya ibada ya Mazishi ya Mtoto Abia . Picha na Fred Cheti.

Siku ya Jumapili Mtoto Abia akiwa na wenzake Sita Majira ya Saa tisa mchana wakiwa wanatoka kanisani aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka na mtoto mwingine aitwae Maria ambae yeye alifariki papo hapo.

Na Fred Cheti.
Hatimae Mazishi ya Mtoto Abia Mtalai (14) ambae alikuwa Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Mlezi aliyefariki kwa kugongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara katika eneo la Kivuko karibu na hospitali ya Mirembe yamefanyika jana.

Ibada ya Mazishi imefanyika katika kanisa kuu la Romani Catholic ambapo katika tukio hilo inaelezwa siku ya Jumapili Mtoto Abia akiwa na wenzake Sita Majira ya Saa tisa mchana wakiwa wanatoka kanisani aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka na mtoto mwingine aitwae Maria ambae yeye alifariki papo hapo huku Mtoto Abia akikimbizwa hospitali na baadae jioni kufariki akipatiwa matibabu.

Mmoja wa wana familia wa Mtoto Abia ambae ni Mjomba wa Marehemu hapa anaeleza historia fupi ya Marehemu hadi umati ulipomkuta.

Sauti ya Mmoja wa wana familia .
Picha ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlezi Mwalimu Anicetus Lymo akizungumza katika ibada hiyo. Picha na Fred Cheti.

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlezi Mwalimu Anicetus Lymo ameelezea kwa masikitiko tukio hilo huku akiwataka Madereva kuzingatia sheria wawapo barabarani ili kupunguza ajali zinazogharimu maisha ya watu.

Sauti ya Mwalimu Anicetus Lymo .

Na Kwa upande wake Diwani katika kata ya Hazina Bwana Samweli Maziba amesema kuwa atafatilia kuhakikisha eneo la kivuko hicho linapatiwa suluhisho la kuduma ili kupunguza ajali zinazotokea katika eneo hilo mara kwa mara.

Sauti ya Bwana Samweli Maziba.