Dodoma FM

Ibihwa watarajia kuondokana na adha ya maji

12 April 2023, 4:46 pm

Boniface Bihemo fundi sanifu Mkuu Ruwasa Bahi.Picha na Bernad Magawa.

Mradi wa maji kata ya Ibihwa unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia RUWASA wilaya ya Bahi na kusimamiwa na kampuni ya Prest Water and Civil works.

Na Bernad Magawa

Mradi mkubwa wa maji unaojengwa katika kijiji cha Ibihwa unatajiwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi ifikapo mwishoni mwa mwezi mei 2023 ili kuwaondolea adha wananchi wa kijiji hicho ambayo iliwatesa kwa muda mrefu.

Akizungumza na kituo hiki katika eneo la mradi huo ambao unajengwa na Kampuni ya Prest water and Civil works ya mkoani Dodoma, Fundi sanifu Mkuu wa RUWASA Wilaya ya Bahi Boniface Bihemo amesema Mradi huo upo katika hatua za mwisho za umaliziaji na unatarajiwa kukamilika muda wowote.

Sauti ya Fundi sanifu Mkuu RUWASA wilaya ya Bahi.
Ofisi ya chombo Cha usimamizi wa mradi wa maji Ibihwa ikiwa katika hatua za umaliziaji.Picha na Bernadi Magawa.

Naye Muwakilishi wa kampuni ya Prest water and Civil works ambao ndio wanaotekeleza mradi huo amesema mradi umechelewa kidogo kukamilika kutokana na kuchelewa kwa kibali cha masamaha wa kodi baada ya kile cha awali kupita muda wake na kuahidi kuwa mapema mwishoni mwa mwezi mei watakabidhi mradi ili wananchi waanze kuutumia.

Sauti ya Muwakilishi wa kampuni ya Prest water and Civil works.

Mradi wa maji kata ya Ibihwa unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia RUWASA wilaya ya Bahi na kusimamiwa na kampuni ya Prest Water and Civil works kwa gharama ya shilingi milioni 709 ukitarajiwa kuhudumia zaidi wananchi 7443 pindi utakapokamilika.