Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwa na desturi ya kufanya mazoezi

15 September 2023, 6:39 am

Picha ni baadhi ya watu wakifanya mazoezi kwaajili ya kuimarisha viungo vya mwili.Picha na Mindi Joseph.

Ikumbukwe kuwa Idara ya Kinga, Wizara ya Afya imeanzisha Mpango kwa watumishi kufanya mazoezi mara mbili kwa wiki siku ya Jumatano na Ijumaa jioni mara baada ya saa za kazi kuanzia saa 9:30 hadi saa 11:00 jioni.

Na Mindi joseph.

Jamii imeaswa kuwa na desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara katika kuimarisha afya ya akili na afya ya mwili hususani kuzuia magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa mjibu wa wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kufanya mazoezi ya mwili inasaidia viungo kuwa vyepesi na kuepusha mwili kupatwa na magonjwa ikiwemo kiurahisi.

Na hapa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga, Wizara ya Afya Dkt. Khalid Massa katika Utekelezaji wa Mpango wa Mazoezi na Afya ya Mwili amesema mazoezi yana umuhimu si tu afya ya mwili bali afya afya ya akili.

Sauti ya Dkt. Khalid Massa.
Mkurugenzi Idara ya Kinga, Wizara ya Afya Dkt. Khalid Massa katika Utekelezaji wa Mpango wa Mazoezi na Afya ya Mwili akiongelea umuhimu wa mazoezi.Picha na Mindi Joseph.

Baadhi ya wananchi jijini dodoma wanakiri kuwa kufanya mazoezi ya mwili kunasaidia kuondoa msongo wa Mawazo.

Sauti za wananchi.

Ikumbukwe kuwa Idara ya Kinga, Wizara ya Afya imeanzisha Mpango kwa watumishi kufanya mazoezi mara mbili kwa wiki siku ya Jumatano na Ijumaa jioni mara baada ya saa za kazi kuanzia saa 9:30 hadi saa 11:00 jioni ikiwa ni hatua kuungana na mkakati endelevu wa Wizara ya Afya wa Kupambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.