Dodoma FM

Wazazi Huzi watakiwa kuto katisha masomo ya watoto wao

6 April 2023, 5:53 pm

Wanafunzi wa shule ya sekondari Huzi.Picha na Michuzi Blog.

Diwani wa kata hiyo anasema suala hilo limeendelea kulichukuliwa hatua kali kwa wazazi wanao jihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Wito  umetolewa kwa wazazi wa Kata ya Huzi Wilaya ya Chamwino kuachana na dhana potofu ya kuwakatisha watoto masomo yao kwa kuwawekea shinikio la kujifelisha mitahni yao ya mwisho.

Diwani wa Kata hiyo Bw.Hosea Chiwanga ameeleza kuwa changamoto hiyo imekuwa ni  kubwa kwa baadhi ya wazazi kuwataka watoto wao kutofanya vizuri katika mitihani yao mwisho.

Sauti ya Diwani wa Kata hiyo Bw.Hosea Chiwanga

Aidha baadhi ya wananchi wa kata ya Huzi wamewashauri wazazi wenye tabia hiyo kuachana na tamaa za kuwaozesha na kuwatumikisha watoto wao kwa manufaa yao na badala yake wawaache watimize ndoto amabazo zitakuwa msaada kwa familia

Sauti za wazazi

Wameongeza kuwa maisha ya sasa yamekuwa ni magumu kwani vijana wengi wameshindwa kuyamudu  hivyo ni vyema Serikali kuwachukulia hatua wazazi wenye tabia hiyo

Esta Yohana ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza amewasihi wanafunzi wenzake kuachana na vishawishi vya wazazi kuwataka kujifelisha pamoja na baadhi ya tamaa za mtaani

Sauti ya Mwanafunzi