Dodoma FM

Kamati ya kutathmini hali ya uchumi katika vyombo vya habari yaongezewa miezi 6

23 May 2023, 3:09 pm

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nauye akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Mindi Joseph.

Kamati hiyo iliyoundwa na Waziri Nape tarehe 24 Januari 2023 sasa itafanya kazi hadi mwezi Novembar 2023 na kuleta mapendekezo ya kushughulikia suala la uchumi kwenye vyombo vya habari.

Na Mindi Joseph.

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nauye ameridhia kuingozea Miezi 6 Kamati ya Kutathimini hali ya uchumi katika vyombo vya habari nchini.

Kamati hiyo ya kuangalia hali ya uchumi kwenye vyombo vya habari awali ilipewa miezi mitatu.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dodoma Waziri Nape amesema wamekubaliana kuongeza miezi 6 kwani serikali inategemea matokeo ambayo yatatoa mwelekeo wa sekta ya habari.

Sauti ya Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari .
Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathimini hali ya uchumi katika vyombo vya habari nchini Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Mindi Joseph.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathimini hali ya uchumi katika vyombo vya habari nchini Tido Mhando amebainisha kuwa katika miezi hiyo 6 watakuwa na majibu yanayositahili ambayo yatatoa mwelekeo tofauti wa tasnia ya habari.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathimini hali ya uchumi katika vyombo vya habari nchini