Dodoma FM

Kingiti waiomba TARURA kuwatengenezea barabara za mitaani

26 May 2022, 9:14 am

Na; Victor Chigwada.

Kukosekana kwa barabara za mitaa katika kata ya Kingiti imekuwa adha kubwa kwa wananchi hivyo wanaiomba mamlaka ya barabara za vijijini TARULA kuwasaidia kuchonga barabara hizo.

Barabara za mitaa Ni muhimu katika jamii kwani zinasaidia kuweka mazingira rafiki pindi inapotokea dharula ya mgonjwa,kifo na hata matukio mbali mbali yanayo hitaji msaada wa gari

Mwenyekiti wa kijiji Cha kingiti Bw.Juliasi Chihuka amesema kuwa Hali hiyo inawakwamisha hata kufanya ujenzi kwani wanahofia endapo upimaji wa barabara utafanyika unaweza kuathili makazi yao

.

Aidha Diwani wa Kata hiyo amesema nje ya barabara za kuingia mtaani lakini wanaishukuru Serikali kwa ukarabati wa barabara kuu ya kata kwa kuwekwa kiwango Cha changalawe

.

Utoaji huduma za matukioa na majanga ya kijamii umekuwa mgumu ikiwa mtaa husika utakosa njia za mawasiliano ya kutoka eneo moja Hadi kingine.