Dodoma FM

Matukio ya uhalifu tishio kwa wakazi wa Nzuguni

23 February 2024, 5:58 pm

Picha ni Mwenyekiti wa mtaa wa Nzuguni Bw. Jackson Mathias. Picha na George John.

Jeshi la Polisi linaombwa kufanya doria za mara kwa mara hasa usiku na jitihada za kuwapata viongozi hawa zinaendelea ili kujua wamechukua hatua gani katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

Na Mindi Joseph.

Matukio ya uhalifu, wizi na kuchomana visu yanatajwa kuongezeka katika kata ya Nzunguni jijini Dodoma katika siku za hivi karibuni.

Ni nini chanzo cha matukio haya? Wananchi wa eneo hilo wanaelezea.

Sauti za wananchi.

Wahusika wa usafirishaji maarufu kama bodaboda ndio wanabebeshwa tuhuma hizi za kufanya uhalifu na huyu ni miongoni wa bodaboda anasema.

Sauti za Maafisa usafirishaji.
Matukio ya uharifu Wizi na Kuchomana Visu yanatajwa kuongezeka kila siku katika Kata hiyo. Picha na George.

Katika mtaa wa Nzunguni B na maeneo ya Mbuyuni matukio ya watu kuchomwa visu mchana kweupe yanaripotiwa kama anavyosimulia aliyefanyiwa tukio hilo.

Sauti ya muhanga aliye chomwa kisu.

Mbali na visa hivyo watu kujeruhiwa kwa kuchomwa visu hapa Mwenyekiti wa mtaa Jackson Mathias anasema.

Sauti ya Mwenyekiti.