Kiteto yafanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya
14 July 2026, 17:39

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndg. Wazo Michael Mwang’onda, ameipongeza Wilaya ya Kiteto kwa jitihada za kudhibiti ulimaji na usafirishaji wa dawa za ,kulevya.
Na Kitana Hamis.
Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 umewasili Wilayani Kiteto mkoani Manyara, ukiwa na jukumu la kukagua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni tatu, huku Wilaya hiyo ikiendelea kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ndedo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mheshimiwa Remidius Mwema, amesema miradi hiyo inalenga kuongeza kasi ya maendeleo na kuboresha huduma kwa Wananchi
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kiteto limetoa taarifa ya mafanikio katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, likieleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2025/2026 limekamata kilogramu 860 za bangi, miche 6,262 ya bangi pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika uzalishaji wa dawa hizo.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndg. Wazo Michael Mwang’onda, ameipongeza Wilaya ya Kiteto kwa jitihada za kudhibiti ulimaji na usafirishaji wa dawa za ,kulevya. Amesema hatua zinazochukuliwa na viongozi, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi zinaonesha dhamira ya kulinda afya na usalama wa jamii.