Dodoma FM
29 June 2026, 17:34

Elizabeth Pagama ni mwana kikundi cha ufugaji amesema wanatumia fursa ya uwepo wa ofisi za taasisi ya TALIRI Kikombo kujua mbinu za ufugaji bora.
Na Stephen Noel .
Zamani ufugaji ulionekana kama kazi ya wanaume tu lakini kadri Siku zinavyozidi kwenda mambo yamebadilika ufugaji unafanywa na jinsia zote Kwa lengo la kujiinua kiuchumi .
Kauli hiyo imetolewa na Dkt Emanuel Lyimo alipokuwa akifingua kikundi cha wanawake waliojikita Katika ufugaji wa kisasa hapa wilayani .
Amesema Ili kuwa na kipato Cha Uhakika Kuku wa kisasa, mbuzi wa maziwa kama Gogo ,lishe,na heshima ni lazima kundi Hilo la kina mama kujikita Katika ufugaji wa kisasa na kuachana na ufugaji wa kienyeji.