Dodoma FM

Unyanyapaa kikwazo cha watu kuweka wazi hali ya afya zao

12 December 2024, 4:43 pm

Picha ni Daktari Martine Kayuli kutoka kituo Cha Afya Makole akiongea na waandishi wa habari .Picha na Fred Cheti.

Aidha ameongeza kuwa vifo vya Watoto vinavyotokana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoani Dodoma vimepungua.

Hofu ya kuogopwa kutengwa katika jamii imeelezwa kuwa chanzo kikubwa kinachowafanya baadhi ya watu kushindwa kuwaweka wazi watu wao wa karibu pindi wanapokutwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.

Baadhi ya wananchi kutoka Mkoani Dodoma wamesema hayo wakati wakifanya mahojiano na Dodoma Tv ambapo wamebainisha sababu ziazowafanya watu kuwa wawazi katika familia zao, pindi wanapogundua wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi jambo ambalo linawafanya baadhi ya watu kupoteza maisha kutokana na kutokupata huduma staiki.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Daktari Martine Kayuli kutoka kituo Cha Afya Makole amesema kuwa bado wanaendelea kuelimisha kwa kutoa taarifa kwa jamii hususani kwa mama wajawazito.

Sauti ya Dkt.Martine Kayuli .