Dodoma FM
Dodoma FM
9 September 2025, 16:35

Aidha, vifo vitokanavyo na kujiua vinashika nafasi ya tatu duniani kwa vijana wenye umri wa miaka 15–29 ambapo zaidi ya asilimia 73 ya vifo hivyo hutokea nchi zenye kipato cha chini na cha kati.
Na Lilian Leopold.
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kuzuia Kujiua Duniani tarehe 10 Septemba imeelezwa kuwa magonjwa yasiyoambukizwa na ugumu wa maisha ni miongoni mwa sababu zinazochangia visa vya watu kujiua.
Hayo yamebanishwa na Mtahu Mtahu Mtaalamu wa Masuala ya Saikolojia ya jamii kutoka Dodoma wakati akizungumza na Taswira ya Habari.
Na je ni makundi yapi yapo hatarin kujiua? Na hapa mwanasaikolojia ameelezea kwa upana zaidi.
Aidha amewataka wananchi hususan makundi rika kutembea vituo vya afya ili kupata ushauru kutoka kwa wataalam wa afya kwa kufanya hivo kupunguza visa vya watu kujiua.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), za mwezi Machi mwaka 2025, kulikuwa na visa vya kujiua zaidi ya 720,000 ambapo wanaume wanaongoza mara mbili zaidi ya wanawake katika matukio hayo.