Dodoma FM

Vikoba vidogo vimekuwa fursa kwa jamii katika kujiwekea akiba

14 August 2026, 16:36

Vikoba fursa za kuwawezesha wananchi kuweka akiba na kupata fedha kwa urahisi kupitia michango ya pamoja.Picha na mtandao.

Bahati Jerome Mwalimu wa vikoba amesema vikoba vina faida kwa sababu vinampa mwanachama nafasi ya kujiwekea akiba kwa urahisi na kupata fedha anapohitaji. Hata hivyo, ameshauri wananchi kujiunga na vikoba vilivyosajiliwa ili kuwa na uhakika wa taratibu na ulinzi wa fedha zao.

Na Saida Athumani.

Vikundi vidogo rasmi vya kuweka na kukopa fedha maarufu kama vikoba vimeendelea kuwa fursa kwa jamii kwa kuwawezesha wananchi kuweka akiba na kupata fedha kwa urahisi kupitia michango ya pamoja.

Taswira ya habari  imetembelea mtaa wa Isanga Jijini Dodoma nakuzungumza na baadhi ya wanachama wa vikoba ambapo wameeleza kuwa vikoba vimewasaidia kuweka akiba, kupata mikopo na kuongeza mitaji ya shughuli zao.

Pia wamezitaja changamoto ikiwemo baadhi ya wanachama kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati na wakati mwingine kusababisha hasara kwa kikundi.

Sauti na Saida Athumani.